Testimonies

Short stories from members who chose to share how God answered prayer. Your own prayer requests stay private unless you publish a testimony here.

pr nashukuru Mungu nilipataka kazi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu na Nina Fanya kwa nguvu zake. pr Mimi ni kijana nilikuwa na mke ambaye nilimpa mimba nipo chuo 2018 nikamwoa 2022 nikaishia nae Kwa miaka miwili badae akanitoroka akaenda kwa mwanaume mwingine bila Mimi kuja. nilitumia garama kumrudisha alipo Rudi arikaa mwaka Moja akatoroka na yule yule mwanaume nimetumia gharama kumtafuta Hadi kupelekana polisi badae akaniambia anitaki nibaki na maisha yangu nisimfutilie Tena. sms yake ni hii (Kwanza mie saivi siyo mke wako sawa tafuta mke mwingine oa make sina latiba yakurudi tena huko siitaji kabisa maswala ya wanaume tena hasa wanaume wahuko muna loho mbaya sijui umenielewa) najikuta nakosa amani nakuwa na sonona na mashaka ya kila ninapomwazia na nilimwahidi Mungu sitakuwa na mwanamke mwingine zaidi yake hivyo pr naomba mniombee aweze kuwa na roho ya kurudi tuishi kama familia ya pamoja tukimsubiri yesu pia awe na roho iliyoturia kwa Mungu na familia yetu. pia ikiwa hatarudi basi anipe roho ya unyenyekevu na hekima niweze vumilia haya yote katika kipindi hiki naomba mniombee sana maana napitia wakati mgumu naamini Mungu atajibu.

Frank Ndimbo · Sep 10, 2026

Nmepata chuo bila nguvu zale nisingeweza

Anonymous · Sep 9, 2026

Amemaliza mitihani salama bila kufeli Amen🥰

Anonymous · Sep 9, 2026

Bwana nimwema hakika nimeona maajabu kurudi hospitali kupiga picha ya xray mguu ulio vunjika mwezi wa saba tarehe moja mpka mwezi wa tisa tarehe moja nimepigwa picha mguu wangu ukaonekana kuwa mfupa mdogo umepona mkubwa picha nikiangalia nikama ya mara ya kwanza ambayo nilipigwa kuonysha haijaunganika lakini nikafunguliwa hakuna maumivu kabisa wakasema niko sawa ulishikana lakini kidogo na kando kiasi basi nikaambiwa kama sina maumivu nirudi nyumbani nianze mazoezi tu pole pole mimi kwangu naona ni muujiza nikiona hiyo picha hakika bwana ameunga mfupa kwa njia apendayo yeye nimeshkuru sana asnte kwa maombi mungu anaweza.maajabu aliyonitendea hata mimi nami nitasimama tena aki nita maisha yangu yote namkabidhi bwana yesu na mimi Asante kwa maombi bwana ametenda aki nimependa nitume izo picha lakini sioni optio ya kutuma picha

Davis manyeso Baya · Sep 1, 2026

Namshukuru MUNGU kwa upendeleo wake kwangu, nimeuona mkono wake wenye nguvu, kwa hali niliyokuwa nayo nilifikia hatua nikakata tamaa kila mtu niliyemfikia niliamini kabisa anaweza kunisaidia na kabla ya kumfata nilichunguza juu ya uwezo wake lakini sikufanikiwa kusaidiwa wengi walinikwepa kabisa, siku moja nisiyoitarajia nilipokea simu saa tano usiku na kuuliza ninaitaji doccument za aina gani tena na mtu ambaye sie muhumini wa kanisa letu, kwakweli niliona nguvu ya MUNGU kabisa, kwa presaure niliyokuwa naye nilisema nani angeweza kunipa nyaraka zake za mhumihu za kifedha kama sio kwa uweza wa MUNGU? maana wengu walinikatisha tamaa wengine waliniambia kwanini uniombe mimi, wengine walishauliwa na mameneja wa benk wasitoe nyaraka zao za kifedha kudhamini mtu kwani sio salama, kwaiyo sikuona njia, lakini MUNGU alifungua njia mahali ambao sikutarajia, tena yeye ndio alikuwa ananikazania nizipate kwa haraka na alionesha ushilikiano mkubwa kila ninacho mwambia ananipa, MUNGU atukuzwe sana katika hili, mimi na familia yetu tumemsifu na kumtukuza MUNGU kwa mkono wake hodari,

Baraka sitta · Aug 28, 2026

Mungu anajibu kwakweli, ila nimejifunza wakati mwingine matokeo ya makosa yako Mungu yanatokea ili uone uchungu wa kukosea

Elishadai · Aug 19, 2026

ninapenda kutoa ushuhuda ya kwamba Bwana amenisaidia nimejifungua salama na wote na mtoto Tupo salama ingawa mtoto alikaa vibaya akatanguliza makalio ilibidi nifanyiwe oparesheni lakini MUNGU aliingilia Kati,,,narudisha shukrani na sofa Kwa MUNGU aliyejuu...nimejifungua Leo tar 01/08/2026,,Kwa majina naitwa MARIAM ABDALLAH

MARIAM ABDALLAH · Aug 1, 2026

Hakika Mungu ametenda kwa kujibu maombi yangu mawili tayari, jina lake litukuzwe

Elishadai · Jul 26, 2026

kuanzisha biashara

Ninamshukuru Mungu sana tena alsana maana sabuni ambayo nilitengeneza ya kwanza wateja waliyinunuwa na nikapata faida. Pastor Mungu amenitendeya makubwa mengi siwezi kunyamanza.Mungu hujibu maombi jamani. Asante sana mchungaji Mungu akubariki na akupe afiya njema.

FADHILI · Jul 21, 2026

namshukuru Mungu maana kweli ufaulu wa watoto wangu uko juu mno jina la Mungu litukuzwe sana

lidya · Jul 14, 2026

Ninamshukuru Mungu wa mbinguni Pr siku ya tarehe 09/07 mwaka huu. niliota ndoto nikiwa nimelala mchana kwamba tulikuwa na wewe kwenye kambi fulani. nikapata nafasi ya kuongea na wewe kitu ambacho ulinambia ni kwamba Kuna kitu kizuri Mungu ameweka ndani ya kinywa changu.. na baada ya mda mchache ukaniuliza tena umenielewa nikajibu nikasema nitaifanya kazi ya Mungu endapo Mungu ataniongoza ukaniambia hicho ndipo ninapaswa kuomba. kiukweli Pr. ndani yangu ninajua nina wito katika kazi ya Mungu lakini sielewi nifanye nini ili Mungu anipatie Mwongozo. ndani yangu Pastor ninahisi kuna nguvu za giza huu ni mwaka wa 4 sasa na sijui nifanye nini mpaka sasa. Naomba unisaidie katika hili.

REBECCA MNIKO SINDA · Jul 13, 2026

ni mkuu na anatend

laila · Jul 10, 2026